NENO LA LEO: 1WAKORINTHO 1: 27 Bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima;

NENO LA LEO: 1WAKORINTHO 1: 27 Bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu.
TAFAKARI: Katika safari ya UKUAJI wa IMANI zetu, tumeitwa ili tumpendeze Mungu peke yake. ULIMWENGU ujapotuona TU wadhaifu, Mungu anaiona NGUVU iliyomo ndani ya IMANI yetu. IMANI aliyotuumbia kwa njia ya NENO lake. IMANI inayoutafuta USO wa Mungu na wala SIYO hekima ya ULIMWENGU huu. Mungu anafurahishwa na IMANI inayoshikamana na AHADI zake kuliko HEKIMA inayopingana na UWEZA wake. Mungu ametuchagua SISI apate kuudhihirishia Ulimwengu, juu ya Nguvu na Uweza alionao dhidi ya “Wenye Hekima” ya kidunia.
SALA: Ee Mwenyezi Mungu, tunakuomba utusaidie ili tuweze kuzifuata AHADI zako siku zote. Utupe NEEMA yako ili tukupendeze Wewe na wala siyo ulimwengu huu, ni katika jina la Yesu Kristo, Amina.
(c)IYK_Neno