Karibuni Ibada ya Kiswahili | Leo Jpili 23 Julia 2017 Kuanzia Saa Kumi Kamili | Mafundisho

Ibada ya Kiswahili – 23 Julai 2017 na Mch. Ipyana Mwakabonga

Usemi wa Wahenga “Samaki mmoja akioza basi wote wameoza”

Salaam kabla ya Mahubiri: “Unataka kufika umbali gani na umejiandaa kiasi gani?!Basi kaa mkao wa kwenda!

Nuhu: Tunajifunza kitu gani kutoka katika somo la Nuhu

Somo: Mwanzo 6:1-22

Mwanzo 6:21 21Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.

Mwanzo5:28-29 28 Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana. 29 Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani Bwana.

Yuda 1:6-76Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. 7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.

Nuhu: Tunajifunza kitu gani kutoka katika somo la Nuhu

Mungu anatusaidia kuboresha mitazamo yetu

  • Tunavikwa uwezo wa kuona na kutambua mitazamo chanya pasipo kujali mazingira tunayoishi
  • Kutujengea utayari wa kuyapokea mafundisho sahihi ambayo yanaweza kuteletea mabadiliko katika maisha yetu!
  • Kutambua thamani ya nafasi yako katika mpango wa Mungu ili uweze kuongezewa…

 

Vizibo/Kizuizi

 

  1. Vinavyoweza kuondolewa
    • Vizibo vya kujiwekea wenyewe
  2. Visivyoweza kuondolewa
  3. Vinavyoletwa na watu

 

IMG_3778

Mahubiri Jumapili 11 Juni 2017 |Mch Ipyana Mwakabonga | Mhubiri 9:16

3 Yohana 1-4 1Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli. 2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3 Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli. 4 Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.

1 Mambo ya Nyakati 4:9-10 9Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. 10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.

Zaburi 78:41  41Wakarudi nyuma wakamjaribu Mungu; Wakampa mpaka Mtakatifu wa Israeli.

Habakuki 2:2-3  2Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. 3 Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.

Mhubiri 9:16 16Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.