NENO LA LEO | ISAYA 51:7-8 Nisikilizeni,ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sharia yangu, msiogope matukano ya watu, wala msifadhaike kwasababu ya dhihaka zao…

ISAYA 51:7-8

Nisikilizeni,ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sharia yangu, msiogope matukano ya watu, wala msifadhaike kwasababu ya dhihaka zao. Maana nondo itawala kama vazi,na funza atawala kama sufu;bali haki yangu itakuwa ya milele,na wokovu wangu hata vizazi vyote.

TAFAKARI

Tunajua kuwa woga na kufadhaika ni kwasababu hatujalishika neno la Mungu na kuliweka moyoni mwetu?.Tunajua kuwa dhihaka na matukano vyote Mungu humshindia yule amwaminie na kulishika neno lake?.Tuweni macho watu wa Mungu na tulishike neno lake.

SALA

Baba katika Jina la Yesu Kristo kipekee tunapokea neno lako takatifu ambalo umependa tulitafakari kwa upya siku ya leo.Tunakuomba utukirimie tuweze kulishika na kulitenda ili tuijue na kuipokea haki yako itakayo tupeleka Mbinguni.Ni katika Jina La Yesu Kristo.Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org