NENO LA LEO: Isaya 61:10 Nitafurahi sana katika Bwana. . .

NENO LA LEO: Isaya 61:10 Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.

TAFAKARI: Mungu mkuu amekufunika na vazi la haki hivyo huna budi kumshangilia. Vazi hili la wokovu la haki ni ishara ya kumshinda shetani. Kuwa mwenye furaha kwa kuwa umemshinda shetani na uzidi kumtegemea Mungu aimarishe mbegu zake za haki na wokovu kwako.

SALA:  Mwenyezi Mungu asante kwa maana umenichagua kuwa miongoni mwa watoto wako uliowavika taji la haki na wokovu. Naahidi kukutumikia siku zote za maisha yangu ukiwa wewe kiongozi wangu. Amen
(c)IYK_Neno
www.iykcolumhus.org