NENO LA LEO | Kutoka 2:23-25 Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa, wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia…

Kutoka 2:23-25

Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo. Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia.

TAFAKARI

Wana wa Israel walikuwa utumwani miaka 430, walizoea hali ya utumwa na kwao ilikuwa kawaida. Ilifika kipindi zile njia zote ambazo walikuwa wanazijua ziliwasadia kustahimili utumwa zilifika kikomo na wakaanza kuugua kwa utumwa wao. Inawezekana umepitia hali fulani ambayo si sawa lakini umezoelea shida yako na umejaribu kila aina ya njia ya kukusadia kustahimili maumivu yako. Imefika wakati maumivu yamekuwa makali sana, huwezi endelea kuvumilia. Wana Israel walipofika katika hali ya kushindwa kuvumilia walilimlilia Bwana, waliomba na kuomboleza mbele zake na Bwana akawasikia. Leo nataka nikutie moyo kuwa jaribu maombi, jaribu kumlilia Mungu. Hajashindwa bado, atakutumia na wewe Musa wako akusadie kutoka katika utumwa ulio nao.

SALA

Mungu wangu, naleta shida yangu. Naleta maumivu yangu mbele zako. Nisadie Mungu, nitokee Baba na nipiganie muumba wangu,unishindie.
Katika jina la Yesu ninaomba , AMEEN.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

Leave a Reply