NENO LA LEO | Luka 10:2 Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache…

Luka 10:2

Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.

TAFAKARI

Unaposoma hili andiko kwenye dunia ya leo unaweza sema kuwa Yesu amejibiwa maombi yake maana siku hizi kuna kanisa katika kila kona na kila mtu anajiita mtumishi wa Mungu. Ni kweli sisi sote ni watumishi wa Mungu lakini si wote tunasimamia kusudi la Mungu katika eneo tulilo wekwa. Kuna wengi wanaonekana wanafanya kazi ya Mungu lakini hawana nia ya kupeleka ufalme wa Mungu mbele bali wapo kwa ajili ya matumbo yao. Tunaweza waiita watumishi wa Mungu hewa ambao hawawikilishi kazi ya Yesu msalabani. Tuombe Mungu atuletee watu watakao tufundisha kuhusu, dhambi, utakatifu, hukumu ijayo na uzima wa milele. Tuombe Mungu atuletee wachungaji watakao hurumia kondoo na kuweza acha yote na kuwatafuta wale waliopotea. Tuombe Mungu alete watenda kazi kwenye shamba lake.

SALA

Mungu Baba, tunaomba ulete watenda kazi watakao simamia kusudi lako katika kanisa lako pasipo kuyumbishwa na kitu chochote. Kwa Jina la Yesu, Amina.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.com

Leave a Reply