NENO LA LEO | Matayo 6:25-26 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi…

Matayo 6:25-26

Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?

TAFAKARI

Hapa duniani tunapita tu na siku zinaenda haraka mno. Katika hii miaka tunayopewa na Mungu huwa tunatumia muda mwingi kusumbuka na vitu vya dunia hii Kama chakula, mavazi na kadhalika. Katika kusumbukia huku mara nyingine huwa tunamweka Mungu pembeni na mara nyingi tunasahau kuwa yeye ana
uwezo wakutupatia kila tunachohitaji kwa sababu vitu vyote ni mali yake.
Siku ya leo nataka nikukumbushe kuwa Kama Mungu huwatunza ndege wa angani na kuwatimizia mahitaji yao,
basi wewe uwe na hakika atakutimizia haja zako na kuhakikisha hatapungukiwa na kitu, (Zaburi 23:1.)

SALA

Bwana Mungu, maisha yangu hapo mbele zako. Naamini utakutana na kila hitaji langu sawa sawa na utajiri wako ndani ya Kristo Yesu Bwana wangu. Kwa Jina la Yesu, Amina.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

Leave a Reply