NENO LA LEO | Matendo 17:28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu…

Matendo 17:28

Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.

TAFAKARI

Kila mmoja wetu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Kuna sauti ya Mungu ndani yako ambayo inakuongoza kufanya mema na kukukataza mabaya. Wengine wanaita dhamiri, wengine wanaita sauti ya Roho Mtakatifu, wengine wanaita machale lakini mwisho wa siku ni Mungu ambaye huongea ndani mwako. Hii ndio ile sauti ambayo inatukanya tunapojisahau na kufuata njia potofu. Hii ndio sauti inayotuhimiza kumtafuta Mungu na kuishi maisha ya kumpendeza. Siku ya leo napenda ufahamu kuwa Mungu yumo ndani yako. Fungua moyo na mpe ruhusa ya kutawala maisha yako. Bado neema ipo usije kubali ndugu yangu kufia dhambini wakati wokovu unapatikana bure.

SALA

Mungu wangu, Asante kwa zawadi yako ya wokovu. Nisadie niweze tembelea kwenye wokovu wako siku zote. Kwa Jina la Yesu, Amina.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org