NENO LA LEO | Methali 19:21 Mna mipango mingi katika moyo wa mwanadamu, lakini shauri la Yehova ndilo litakalosimama…

Methali 19:21

Mna mipango mingi katika moyo wa mwanadamu, lakini shauri la Yehova ndilo litakalosimama.

TAFAKARI

Najua leo asubuhi umeamka ukiwa na mipango mingi kwa ajili ya siku ya leo, wiki hii, na hata mwaka mzima. Ni kitu kizuri kuwa na mipango lakini mara nyingi tunashindwa kukumbuka kuwa kuna mpango wa Mungu katika maisha yetu pia. Nataka nikukumbushe kuwa ni vizuri kumshirikisha Mungu katika mipango yako na kumwomba akuongoze kutokana na mapenzi yake. Wafilipi 4:13 “Nitafanya yote kupitia yeye anitiaye nguvu”.
Katika yote ufanyayo ujue shauri lake(Mungu) litasimama na yeye atatukuzwa maishani mwako ukiweka mipango yako mbele zake.

SALA

Mungu Baba, nakabidhi mipango yangu yote kwako. Naomba yale uliyokusudia yapate simama sawa sawa na mapenzi yako. Kwa Jina la Yesu, Amina.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

Leave a Reply