NENO LA LEO | Mhubiri 7:1 Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu…

Mhubiri 7:1

Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.

TAFAKARI

Leo napenda kugusia kidogo hiki kipengele cha mtu kuwa na hasira za haraka haraka. Kuna wengi wetu ni wepesi kukasirika, pindi tushikwapo na hasira hujikuta tunafanya maamuzi ambayo tunakuja kujutia baadaye. Biblia inatufundisha kuwa tusiwe wepesi wa kukasirika maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu. Kwa maneno mengine kipindi tunapokuwa wepesi wa kukasirika bila hata sababu ya msingi maandiko yanatuweka katika kundi la wapumbavu. Imetupasa kumwomba Mungu atusadie katika eneo hili; atupe uvumilivu wa ndani ili tuweze kutawala roho zetu kipindi makwazo yajapo.

SALA

Mungu wangu na Baba yangu, naomba nisamehe kwa pale nilipokasirika visivyo haki; naomba nisadie niweze kutawala roho yangu kipindi nikwazwapo. Kwa Jina la Yesu, Amina.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org