NENO LA LEO | MUHUBIRI 5:2 Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu. Kwa maana,Mungu yuko mbinguni na wewe uko chini…

MUHUBIRI 5:2

Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu. Kwa maana,Mungu yuko mbinguni na wewe uko chini, kwahiyo maneno yako na yawe machache.

TAFAKARI

Wapendwa katika Kristo!hebu tumia dakika 5 kutafakari kwanini Mungu ametuletea hili neno DUNIANI.Neno limeanza kwa kuonya kuwa USISEME maneno ya UJINGA.Hii ni kwasababu Mungu anajua kuwa tumekuwa tukiongea maneno Mengi bila kujiuliza kuwa yana maana gani mbele za Mungu.Mungu anasema yeye yuko Mbinguni sisi tuko CHINI.Neno chini lina maana kubwa SANA.Inatupasa sisi tulioko chini tutii yale Mungu anayohitaji tuyafanye.Tusiwe wepesi kusema jambo lolote bila kujua maana yake mbele za MUNGU.

SALA

Mungu wetu uishie mbinguni.Tunakuomba utusamehe dhambi zetu,hasa pale ambapo tumekuwa tukisema maneno mengi bila kujali kama yanakupendeza.Pia tunaomba utujalie tutii maagizo yako.Ni katika jina la Yesu Kristo tumeomba.Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org