NENO LA LEO | ZABURI 20:1-2 BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu pake…

ZABURI 20:1-2

BWANA akujibu siku ya dhiki,Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.Akupelekee msaada toka patakatifu pake.

TAFAKARI

Neno linatuambia bwana ANAJIBU,pia linasema kwa wakati fulani mtu anaweza kufikwa na DHIKI.Neno dhiki ni pana na ni gumu pia kwetu binadamu pale linapotufika .Watu wa Mungu tumezungukwa na DHIKI katika maisha yetu,na wale ambao haijawafika bado inabidi kumshukuru sana Mungu na kumuomba sana ili atuepushe au atujibu pale inapotufika.Kila mtu anajua ni wapi,wakati gani,kwenye nini DHIKI inamtesa.Tukumbuke Biblia inatuambia”Ombeni lolote kwa IMANI nanyi mtapewa”.Jambo lolote linalokusumbua AMINI kwanza kuwa Mungu amesha kushindia kisha Omba kwa BIDII.”Utapewa”.Mungu hutoa MSAADA kutoka PATAKATIFU pake.

SALA

Mungu tunakuomba utushindie dhiki zetu.utukumbushe kuwa hakuna GUMU linalokushinda.Tunajiweka mikoni mwako tukiamini umesha tenda.Katika jina la mwanao Yesu Kristo tumeomba,Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org