NENO LA LEO | ZABURI:27:4 Neno moja nimelitaka kwa BWANA,Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA siku zote za maisha yangu…

ZABURI:27:4

Neno moja nimelitaka kwa BWANA,Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA siku zote za maisha yangu. Niutazame uzuri wa BWANA Na kutafakari hekaluni mwake.

TAFAKARI

Hapa Neno linazungimzia kutafuta KUKAA nyumbani mwa BWANA,na siyo tu kukaa nyumbani mwa bwana ila kukaa SIKU zote za maisha ya mwanadamu.Ndugu zangu njia PEKEE ya kumtumikia Mungu ni kukaa NDANI ya nyumba yake.Nyumbani hakuna AINA yoyote ya Dhambi.Hivyo watu wamungu tutafuteni kukaa nyumbani mwa BWANA.

SALA

Mungu mwema tunaomba utukumbushe kujitakasa na kisha kurudi kukaa ndani ya nyumba yako milele.Ni katika Jina la Bwana wetu Kristo Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org