NENO LA LEO | Mithali 10:1 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye, Bali mwana mpumbavu ni mzigo kwa mamaye…

Mithali 10:1

Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye;Bali mwana mpumbavu ni mzigo kwa mamaye.

TAFAKARI

Hekima huzaa matunda mema mbele za Mungu Bali upambavu ni mzigo mbele za Mungu.Biblia inasema watu wa Mungu tunatakiwa tuenende kwa hekima katika kila jambo tunalofanya hapa Duniani.Pia Biblia inasema kilichokubalika duniani na mbinguni kimekubalika.hivyo watu wa Mungu tunapaswa kutokuwa mizigo au wapumbavu,zaidi tunapaswa kumfurahisha Mungu wetu kwa kufuata maagizo yake.

SALA

Baba yetu,Mungu wetu,mfalme wetu,tunasogea mbele zako tukiamini uweza na mamlaka yako juu yetu.Tunajiachilia mikononi mwako tukiomba utubadili ili tuishi maisha yetu kwa hekima na sio kuwa wapumbavu.Katika Jina la Yesu Kristo tumeomba.Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | Mithali 7:1-2 Mwanangu,yashike maneno yangu,Na kuziweka amri zangu akiba kwako.Uzishike amri zangu ukaishi,Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako…

Mithali 7:1-2

Mwanangu,yashike maneno yangu,Na kuziweka amri zangu akiba kwako.Uzishike amri zangu ukaishi,Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako.

TAFAKARI

Watu wa Mungu tunaambiwa kuyashika maneno ya MUNGU na kuweka akiba AMRI za MUNGU,huku tukiambiwa wazi kuwa kama tukizishika AMRI za MUNGU na kuzitenda tutaishi.Wapendwa tumrudieni MUNGU ni mkuu sana.Ukizitafakari hizi AHADI zake kwetu,ni kuu sana ila mara nyingine tunajisahau na kumkosea MUNGU wetu.Tutubu na kurudi kwake.

SALA

Mungu wetu mara nyingine kwa sababu ya mahangaiko ya hapa Duniani,tumekuwa tunakukosea bila hata kujijua.Tunakuomba utusamehe na kutukumbusha kuzishika AMRI zako na maneno yako ili tuendelee kuishi. Ni katika Jina la Yesu Kristo tumeomba Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | LUKA 6:20 Akainua macho yake, akawatazama wanafunzi wake, akasema, Heri ninyi mlio masikini, kwasababu ufalme wa Mungu ni wenu…

LUKA 6:20

Akainua macho yake,akawatazama wanafunzi wake,akasema,Heri ninyi mlio masikini,kwasababu ufalme wa Mungu ni wenu.

TAFAKARI

Kuna wakati mambo ya maisha yetu yanapokuwa hayaendi vizuri,kuna uwezekana wa kukata tamaa na kupunguza au kuacha kumtumikia Mungu kwa bidii.Neno hili linaonesha jinsi Bwana wetu YESU Kristo alivyowabariki wanafunzi wake pamoja na wao kuwa masikini.Neno HERI ni neno lenye ujumbe mkubwa SANA wa kubariki.

SALA

Bwana wetu YESU Kristo,mwenye uweza,mamlaka,nguvu,upendo usiyefananishwa na chochote.Tunakushukuru kwa NENO lako lenye kutukumbusha kuwa pamoja na umasikini wetu,ila tunakiwa tuendelee kukutegemea wewe milele.Ni katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo,tumeomba.Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | Yohana 15: 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu…

Yohana 15: 4

Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.

TAFAKARI

Maisha yetu ya Ukristo yanategemea sana mahusiano yetu na Kristo mwenyewe. Tunapokuwa tuna mahusiano mazuri na Bwana wetu Yesu Kristo ndipo hata Ukristo wetu unakuwa imara siku hadi siku. Pindi mahusiano yanapo zorota basi tunampa nafasi adui kuingia na kutushambulia. Inawezekana umekuwa ukijuuliza kwa nini shetani amekuwa akijiinua sana katika maisha yako na maisha ya wale uwapendao. Labda umejaribu kuomba, kukemea na hata kufunga lakini huoni majibu. Leo hii nataka nikukumbushe kuwa kabla hujapigana vita yeyote na yule mwovu; angalia kwanza mahusiano yako na Mungu wako. Tengeneza chochote ambacho kimeharibika kati ya wewe na Bwana Yesu. Kisha mwamini yeye kukufungulia milango yeyote iliyofungwa katika maisha yako.

SALA

Baba katika Jina la Yesu, natamani niendelee kukaa ndani yako, ili na wewe upate kukaa ndani yangu. Nataka nipate kuzaa matunda yaliyo mema mbele zako na kumshinda yule mwovu shetani. Nipatie neema niweze kutimiza hayo yote ninayoyatamani ili jina lako lipate kutukuzwa kupitia maisha yangu. Kwa Jina la Yesu, Amina.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | Zaburi 121:1-2 Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi…

Zaburi 121:1-2

Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi.

TAFAKARI

Mungu ndiye aliye muumba mwanadamu, alituumba mimi na wewe kwa sura na mfano wake. Akatupa dunia ili tupate kuitawala na kuimiliki. Tulipoanguka katika dhambi alimtuma mwanae wa pekee Yesu Kristo ili aje kutukomboa na kuturudisha kwenye nafasi ambayo shetani alichukua. Huyu Mungu ndiye msaada wetu, yeye pekee ndiye kimbilio letu na faraja yetu. Inawezekana ndugu unapitia katika majaribu, inawezekana umeamka asubuhi ya leo ukiwa na mawazo mengi sana ulitamani usiku uwe mrefu zaidi. Nataka nikutie moyo kuwa yupo Mungu. Yupo alikuweka hapa duniani, hajakuweka kwa bahati mbaya na yupo tayari kukusadia kwenye shida yako. Nenda mkimbilie yeye siku ya leo.

SALA

Mungu Baba, uliye mbinguni Jina lako litukuzwe siku ya leo. Naleta shida zangu mbele zako. Unajua yote nayopitia, naomba unitende muujiza siku ya leo nipate kuona mkono wako maishani mwangu. kwa Jina la Yesu nimeomba, Amina

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org