NENO LA LEO | Luka Mtakatifu 21:1 Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina. Akamuona MJANE mmoja akitia mle senti mbili. Akasema…

Luka Mtakatifu 21:1

Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina.Akamuona MJANE mmoja akitia mle senti mbili. Akasema, hakika nawaambia huyu MJANE masikini ametia zaidi kuliko wote.

TAFAKARI

Hapa tunajifunza jinsi utoaji unavyotofautiana.Wakristo ni vyema kuwa watoaji hata kama tunadhani kile tunachomtolea Mungu ni kidogo sana machoni mwetu.Mungu huwa anaangalia moyoni mwa MTU pale anapotoa sadaka.Na kama MTU umebarikiwa kifedha basi ni vyema kumtolea Mungu kulingana na jinsi alivyo kubariki.

SALA

Mungu baba tunaomba utukumbushe juu ya matoleo yetu,tusitoe ziada ya vile ulivyotubariki kwavyo,bali tutoe kulingana na AGIZO lako.Tumeomba katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.Amen!

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | Warumi 2:1 Kwa hiyo, wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru, kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia…

Warumi 2:1

Kwa hiyo, wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru, kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia, kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale.

TAFAKARI

Kuna wakati watu wa Mungu tunajisahau na kuhukumu.Yatupasa tuache kwani hakuna aliyeruhusiwa kuhukumu isipokuwa Mungu mwenyewe.hivyo tuacheni kuhukumu.

SALA

Mungu tunakuomba utusamehe pale tulikojichukulia majukumu yako,tukawahukumu wengine.Tunaomba utukumbushe juu ya hili neno lako.Katika jina la Yesu Kristo tumeomba.Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolimbus.org

NENO LA LEO | 1Yohana 2:18 Watoto,ni wakati wa mwisho; na kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo…

1Yohana 2:18

Watoto,ni wakati wa mwisho; na kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja,hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo.

TAFAKARI

Hapa tunaambiwa kuhusu siku za mwisho kwamba wapinga Kristo watakuja.Watu wa Mungu tukumbukeni kuwa Biblia inasema,neno la Mungu halitapita bure,na pia inasisitiza kuwa neno la Mungu ni kweli.Sasa basi,pamoja na jinsi watu wa Mungu tulivyo na mambo mengi yakufanya hapa Duniani,tusisahau kuwa jambo la msingi sana ni kulishika neno la Mungu,na kukesha tukisali

SALA

Mungu wetu,asante kwa neno lako zuri,asante pia kwa kutukumbusha kuwa siku za mwisho za wewe kuja kulinyakua kanisa zimekaribia.Tunakuomba utukumbushe kuishi ndani yako,na pia kukesha kwa ajili ya kukusubiri.Amen

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | Zaburi 27:1 BWANA in nuru yangu na wakovu wangu, nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani…

Zaburi 27:1

BWANA in nuru yangu na wakovu wangu, nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?

TAFAKARI

Haya ni maswali ambayo watu wa Mungu tunapaswa tujiulize na kuyajibu. Katika maisha wengi wameshindwa kufuata ama kufanya yaliyo mazuri na yenye kuwabariki wao na Mungu kwa sababu tu hawajaliweka NENO la Mungu ndani yao.Tumekuwa tunaishi kwa hofu sana.Hebu tusome upya hii AHADI kisha tujiweke huru kwani Mungu anatupenda sana.Hatuna haja ya kingine zaidi ya upendo wa Mungu.

SALA

Mungu baba mwenye huruma na upendo,usiyeshindwa na lolote,wewe uliye kila kitu,tunakushukuru kwa kutukumbusha kutohifia au kuogopa jambo lolote.Tunaomba utuimarishe mioyoni mwetu ili tuishi ndani ya ahadi hii toka kwako. Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org