NENO LA LEO | Warumi 2:1 Kwa hiyo, wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru, kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia…

Warumi 2:1

Kwa hiyo, wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru, kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia, kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale.

TAFAKARI

Kuna wakati watu wa Mungu tunajisahau na kuhukumu.Yatupasa tuache kwani hakuna aliyeruhusiwa kuhukumu isipokuwa Mungu mwenyewe.hivyo tuacheni kuhukumu.

SALA

Mungu tunakuomba utusamehe pale tulikojichukulia majukumu yako,tukawahukumu wengine.Tunaomba utukumbushe juu ya hili neno lako.Katika jina la Yesu Kristo tumeomba.Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolimbus.org

NENO LA LEO | 1Yohana 2:18 Watoto,ni wakati wa mwisho; na kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo…

1Yohana 2:18

Watoto,ni wakati wa mwisho; na kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja,hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo.

TAFAKARI

Hapa tunaambiwa kuhusu siku za mwisho kwamba wapinga Kristo watakuja.Watu wa Mungu tukumbukeni kuwa Biblia inasema,neno la Mungu halitapita bure,na pia inasisitiza kuwa neno la Mungu ni kweli.Sasa basi,pamoja na jinsi watu wa Mungu tulivyo na mambo mengi yakufanya hapa Duniani,tusisahau kuwa jambo la msingi sana ni kulishika neno la Mungu,na kukesha tukisali

SALA

Mungu wetu,asante kwa neno lako zuri,asante pia kwa kutukumbusha kuwa siku za mwisho za wewe kuja kulinyakua kanisa zimekaribia.Tunakuomba utukumbushe kuishi ndani yako,na pia kukesha kwa ajili ya kukusubiri.Amen

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | Zaburi 27:1 BWANA in nuru yangu na wakovu wangu, nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani…

Zaburi 27:1

BWANA in nuru yangu na wakovu wangu, nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?

TAFAKARI

Haya ni maswali ambayo watu wa Mungu tunapaswa tujiulize na kuyajibu. Katika maisha wengi wameshindwa kufuata ama kufanya yaliyo mazuri na yenye kuwabariki wao na Mungu kwa sababu tu hawajaliweka NENO la Mungu ndani yao.Tumekuwa tunaishi kwa hofu sana.Hebu tusome upya hii AHADI kisha tujiweke huru kwani Mungu anatupenda sana.Hatuna haja ya kingine zaidi ya upendo wa Mungu.

SALA

Mungu baba mwenye huruma na upendo,usiyeshindwa na lolote,wewe uliye kila kitu,tunakushukuru kwa kutukumbusha kutohifia au kuogopa jambo lolote.Tunaomba utuimarishe mioyoni mwetu ili tuishi ndani ya ahadi hii toka kwako. Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | Yohana Mtakatifu 15:9. Kama vile baba alivyonipenda mimi,nami nilivyowapenda ninyi,kaeni katika PENDO langu…

Yohana Mtakatifu 15:9.

Kama vile baba alivyonipenda mimi,nami nilivyowapenda ninyi,kaeni katika PENDO langu.

TAFAKARI

Tunaona jinsi Mungu alivyompenda bwana Yesu,na Bwana Yesu anavyotupenda sisi.Swali linakuja je sisi tunapendana ?,na kama tunapendana je,tunaishi ndani ya PENDO.Tumeagizwa tupendane,na sio ombi bali ni agizo,hivyo yatupasa tulifuate agizo.

SALA

Bwana Yesu asante kwa agizo lako ZURI juu yetu.Wengi tumejisahau na kudhani maisha ya Duniani yako mikononi mwetu na kusahau AGIZO la sisi kupendana.Tunaomba uingie mioyoni mwetu ubadilishe mbegu mbaya zisizo za Upendo na kutufanya tuishi ndani ya hilo PENDO.Katika jina LA Yesu tumeomba na tukisema Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org