Mahubiri Jumapili 11 Juni 2017 |Mch Ipyana Mwakabonga | Mhubiri 9:16

3 Yohana 1-4 1Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli. 2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3 Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli. 4 Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.

1 Mambo ya Nyakati 4:9-10 9Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. 10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.

Zaburi 78:41  41Wakarudi nyuma wakamjaribu Mungu; Wakampa mpaka Mtakatifu wa Israeli.

Habakuki 2:2-3  2Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. 3 Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.

Mhubiri 9:16 16Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.

NENO LA LEO | Zaburi 89:7 Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu, Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka…

Zaburi 89:7

Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu, Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka.

TAFAKARI

Tunasoma katika kitabu cha Ufunuo kuwa kuna viti ishirini na vine vimezunguka kiti cha enzi, na juu ya vile viti kuna wazee ishirini na wanne, na pande zote za kile kiti cha enzi cha Mungu, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma ambao wote pamoja na wazee ishirini na wanne humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, Ufunuo 4. Kama hawa wazee ambao Biblia inasema wamevikwa mavazi maupe, na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu humsujudia Mungu mchana na usiku. Swali linakuja kwako mimi na wewe ndugu yangu, je, tunamwogopa Mungu kama itupasavyo na kumhofu kwenye maisha yetu? Je, Mungu kwetu ni nani? Tunampa nafasi katika maisha yetu au tunamchukulia kawaida sana?

SALA

Mungu wangu naomba nisamehe kwa pale niliposhindwa kuishi sawa sawa na Neno lako. Nisadie niweze kutembea kwenye hofu yako, nipe kukuogopa na kutii Neno lako kuliko kitu chochote katika maisha yangu. Kwa Jina la Yesu, Amina.

©IYK-NENO
www.iykcolimbus.org

NENO LA LEO | 1 Timotheo 4:10 Kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa waaminio…

1 Timotheo 4:10

Kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa waaminio.

TAFAKARI

Mungu wetu anaishi, mkono wake ni mkuu sana. Mzaburi Daudi anasema, Mkono wako ni mkono wenye uweza, Mkono wako una nguvu, Mkono wako wa kuume umetukuka, Zaburi 89:13. Mtume Paul anasema kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai. Siku ya leo nataka nikukumbushe kuwa Mungu wetu yu hai na mkono wake ni mkuu sana. Hakuna jambo linaloweza kumshinda, kinachotakiwa ni kumwendea kwa imani na utaona wokovu wake.

SALA

Mungu wangu, naweka tumaini langu kwako. Naomba uzidi kujifunua kwangu kila iwapo leo ili nipate kukufahamu zaidi. Kwa Jina la Yesu, Amina.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | Ayubu 22:21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia…

Ayubu 22:21

Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.

TAFAKARI

Mzaburi Daudi katika Zaburi 119:165 anasema, “Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza.” Amani ya kweli inapatikana kwa kumjua Mungu, hapatikani kwa kuwa mkristo tu. Unaweza ukawa mkristo na hata ukasema umeokoka lakini usiwe na amani ya kweli moyoni mwako. Ukitaka amani ndani mwako inabidi umruhusu Yesu awe kiongozi wa maisha yako. Inabidi usalimishe maisha yako na kila kitu katika maisha yako mbele zake. Mpe yeye nafasi awe kiongozi wa maisha yako, mtwike mizigo yako yote na ndipo atakupa amani ipitayo fahamu zote ndani ya moyo wako.

SALA

Mungu wangu, naomba amani yako ndani ya maisha yangu. Nasalimisha kila kitu changu mikononi mwako. Nisadie niweze kukutegemea wewe siku zote. Kwa Jina la Yesu, Amina.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | Zaburi 90:10-12 Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini, Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara…

Zaburi 90:10-12

Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara. Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako? Na ghadhabu yako kama ipasavyo kicho chako? Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima.

TAFAKARI

Kila mmoja wetu ameumbwa kwa kusudi. Hakuna ambaye ameumbwa kwa bahati mbaya. Mungu alikujua kabla hujazaliwa, Yeremia 1:5 na pia alitenga wakati maalumu utakaoishi kwenye dunia hii Esta 4:14. Mhubiri 11 inasema kila jambo na wakati wake, kuna mwanzo wa jambo na mwisho wake. Hata kipindi cha kuishi kwetu hapa duniani kimehesabiwa, kwa hiyo imetupasa kuishi maisha ya kumwogopa Mungu ili tupate kutimiza kusudi la kuumbwa kwetu.

SALA

Mungu wangu, nisadie nipate kufahamu kusudi la kuumbwa kwangu na niweze kuishi maisha yangu yote kulitimiza hilo kusudi. Kwa Jina la Yesu, Amina.

©IYK- NENO
www.iykcolumbus.org