NENO LA LEO | MATHAYO 26:31 Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu, kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika…

MATHAYO 26:31

Ndipo Yesu akawaambia,Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu;kwa kuwa imeandikwa,Nitampiga mchungaji,na kondoo wa kundi watatawanyika.

TAFAKARI

Wapendwa watu wa Mungu,Bwana Yesu Kristo asifiwe.Tunaona katika neno la leo jinsi Bwana wetu Yesu Kristo anavyo waambia wanafunzi wake juu ya machukizo watakayo kutana nayo sababu ya makuu alokuwa akiyatenda Bwana Yesu.cha kujifunza hapa ni kwamba hata tukiwa na wema wa kiasi gani kuna WAKATI pamoja na wema wetu bado tunaweza kuhukumiwa.Na pia kuna uwezekano wa kuhukumiwa pasipo sisi binafsi kutenda jambo lolote baya.Tunaona,japokuwa Bwana Yesu hakutenda dhambi lakini wanafunzi wake walichukizwa kwa ajili ya Bwana Yesu.Wakristo tusimame imara katika kumtegemea Mungu.Tujue wazi kuwa hata katika kumtegemea yeye tutafikia wakati tutachukuzwa na wasio mtegemea.

SALA

Mungu Baba asante kwa wema wako wapekee hata tumeweza kuiona siku ya leo.hatuna budi kukushukuru kwa kila jambo Kwa sababu ya ukuu wako.Tunakuomba utupe neema na kutufunulia kujua kwamba pamoja na kukutegemea bado tutachukizwa na wasio kutegemea.Ila tunakuomba utujalie tuweze kusimama imara ndani yako kwa kila jambo hata kama ni jaribu ili mwisho wa yote tuurithi uzima wa milele.Ni katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo tumeomba.Amen

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | Isaya 43:2-3 “Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe na katika mito, haitakugharikisha, uendapo katika moto, hutateketea…

Isaya 43:2-3

“Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. Maana mimi ni BWANA, Mungu wako….”

TAFAKARI

BWANA Yesu anakuhakikishia kwamba atakuchunga siku zote za maisha yako endapo utaamua kumtumikia yeye. Atakulinda na mabaya ya aina yote ambayo mwanadamu pekee kwa kutumia akili zake hawezi. Hebu amini ulinzi huu usio na kikomo na anza sasa kumtumiakia yeye.

SALA

Mwenyezi Mungu baba wa rehema, kwa kupitia mwanao mpendwa Yesu Kristo nimeona ukiniokoa na mambo mengi. Umenipitisha katika magumu mengi na bila wewe kuwa mchungaji nina hakika nisingeweza kuyashinda majaribu haya. Naomba uzidi kutawala maisha yangu na kunitumia siku zote BWANA, Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | MARKO 12:30-31. Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote…

MARKO 12:30-31

Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,na kwa roho yako yote,na kwa akili zako zote,na kwa nguvu zako zote.Na amri ya pili ndiyo hii,Mpende jirani yako kama nafsi yako.Hakuna amri nyingine iliyo kuu zaidi ya hizi.

TAFAKARI

Watu wa Mungu tunakumbushwa kumpenda Bwana Mungu wetu zaidi ya chochote.Swali linakuja kwamba,je,ni kweli ndivyo tunavyofanya?Na kama sivyo tunavyofanya, je hatudhani kuwa tunatakiwa kumpigia Mungu magoti na kumuomba atusamehe na kisha kuanza mara moja kumpenda yeye kama alivyo agiza?.Watu wa Mungu,kumpenda Mungu ni lazima,hivyo hatuna budi kumpenda Mungu wetu.Kisha atatupa yaliyo mahitaji yetu.Pia andiko linatukumbusha kuwapenda jirani zetu kama nafsi zetu,hilo ni agizo kutoka kwa Mungu.Hivyo hatuna budi pia kuwapenda jirani zetu.Wakristo,tutii haya maandiko ili Mungu aweze kuingia kwenye maisha yetu na kuyabadili yawe sawasawa na kusudi la yeye kutuumba na kutuleta DUNIANI.

SALA

Baba Mungu neno lako ni taa na uzima katika maisha yetu.Tukikaa kwako na kutii maagizo yako basi tunauhakika wakuyashinda yote yaliyo magumu ndani yetu.Tunakuomba utujalie kuyashika na kuyatenda yaliyo maaagizo yako.Ni katika Jina la Bwana wetu Kristo tumeomba.Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org