NENO LA LEO | Isaya 43:2-3 “Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe na katika mito, haitakugharikisha, uendapo katika moto, hutateketea…

Isaya 43:2-3

“Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. Maana mimi ni BWANA, Mungu wako….”

TAFAKARI

BWANA Yesu anakuhakikishia kwamba atakuchunga siku zote za maisha yako endapo utaamua kumtumikia yeye. Atakulinda na mabaya ya aina yote ambayo mwanadamu pekee kwa kutumia akili zake hawezi. Hebu amini ulinzi huu usio na kikomo na anza sasa kumtumiakia yeye.

SALA

Mwenyezi Mungu baba wa rehema, kwa kupitia mwanao mpendwa Yesu Kristo nimeona ukiniokoa na mambo mengi. Umenipitisha katika magumu mengi na bila wewe kuwa mchungaji nina hakika nisingeweza kuyashinda majaribu haya. Naomba uzidi kutawala maisha yangu na kunitumia siku zote BWANA, Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | MARKO 12:30-31. Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote…

MARKO 12:30-31

Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,na kwa roho yako yote,na kwa akili zako zote,na kwa nguvu zako zote.Na amri ya pili ndiyo hii,Mpende jirani yako kama nafsi yako.Hakuna amri nyingine iliyo kuu zaidi ya hizi.

TAFAKARI

Watu wa Mungu tunakumbushwa kumpenda Bwana Mungu wetu zaidi ya chochote.Swali linakuja kwamba,je,ni kweli ndivyo tunavyofanya?Na kama sivyo tunavyofanya, je hatudhani kuwa tunatakiwa kumpigia Mungu magoti na kumuomba atusamehe na kisha kuanza mara moja kumpenda yeye kama alivyo agiza?.Watu wa Mungu,kumpenda Mungu ni lazima,hivyo hatuna budi kumpenda Mungu wetu.Kisha atatupa yaliyo mahitaji yetu.Pia andiko linatukumbusha kuwapenda jirani zetu kama nafsi zetu,hilo ni agizo kutoka kwa Mungu.Hivyo hatuna budi pia kuwapenda jirani zetu.Wakristo,tutii haya maandiko ili Mungu aweze kuingia kwenye maisha yetu na kuyabadili yawe sawasawa na kusudi la yeye kutuumba na kutuleta DUNIANI.

SALA

Baba Mungu neno lako ni taa na uzima katika maisha yetu.Tukikaa kwako na kutii maagizo yako basi tunauhakika wakuyashinda yote yaliyo magumu ndani yetu.Tunakuomba utujalie kuyashika na kuyatenda yaliyo maaagizo yako.Ni katika Jina la Bwana wetu Kristo tumeomba.Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | MARKO MTAKATIFU.1:32-34. Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo. Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni…

MARKO MTAKATIFU.1:32-34

Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa,walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi,na wenye pepo.Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni.Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali,akatoa pepo wengi,wala hakuwaacha pepo kunena,kwasababu walimjua.

TAFAKARI

Je WAKRISTO tunajua kuwa hakuna jambo lolote gumu ambalo Bwana wetu Yesu Kristo hawezi kulishinda?.Sisi binadamu tuna elemewa na mambo mengi sana magumu,ila tujue wazi kuwa Bwana wetu Yesu Kristo anauwezo wakuyamaliza KABISA.Kinachotakiwa ni kuleta shida zetu kwake.Shida zetu haziwezi kuushinda ukuu wa Yesu Kristo.Kwenye neno tunaona MAPEPO yameshindwa kunena kwani yanamjua Bwana Yesu.Hata magonjwa tuliyonayo,tukijitoa na kurudi kwa Bwana Yesu,kwa kusali,kuacha DHAMBI,na kushika kila maagizo tuliyo agizwa hapa Duniani,hakika tutapona magonywa, na kamwe hatutakuwa na taabu za aina yoyote.

SALA

Asante Mungu wetu kwa uhai.Asante kwa neema ya kila jambo jema uliloruhusu lifanyike kwenye maisha yetu. Hakuna wakulinganishwa wala kufananishwa na wewe. Tunakupenda sana,na bila wewe hatuwezi kuyashinda magonjwa na dhiki za dunia hii. Tunakuomba utuponye magonjwa,na utujalie kukaa ndani yako kwa utakatifu ili tuondokane na dhiki za Dunia hii. Ni katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, tumeomba. Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org