NENO LA LEO | YOHANA MTAKATIFU 12:44-46 Naye Yesu akapaza sauti, akasema ,Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka…

YOHANA MTAKATIFU 12:44-46

Naye Yesu akapaza sauti,akasema,Yeye aniaminiye mimi,haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka.Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka.Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu,ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani

TAFAKARI

Tunaona sababu ya Bwana yesu kuja katika maisha yetu ni ili yeyote aliye gizani na akaamua kuja kwa Bwana Yesu basi ataingia NURUNI.Neno NURU lina uzito mkubwa sana kwenye maisha yetu watu wa Mungu.Tukumbuke tu kuwa bila nuru hatuwezi kuona,na hivyo mtu ambaye hajampokea Bwana Yesu ni kama amezuiwa na GIZA na haoni chochote.Wakristo hebu tulinganishe GIZA linalokuwepo ndani ya nyumba zetu wakati wa USIKU , na NURU inayotokea tunapowasha taa .Kimsingi kama hatutawasha taa hatutaona kitu.Hivyo basi turudini NURUNI kwa kumpokea Bwana wetu Yesu katika maisha yetu.

SALA

Bwana wetu Yesu Kristo,asante kwa kuwa nuru ya maisha yetu.Wengi wetu tumefungwa kujua kuwa tuko gizani na hatujui namna ya kuiona nuru.Tunakuomba uje katika maisha yetu na kufanyika nuru ili tuweze kuona tena.Bila wewe maisha yetu hayana maana.Ni katika jina la Yesu Kristo tumeomba.Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | MITHALI 8:17-18 Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia…

MITHALI 8:17-18

Nawapenda wale wanipendao,Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.Utajiri na heshima ziko kwangu,Naam,utajiri udumuo,na haki pia.

TAFAKARI

Mungu huwapenda wale wampendao,na ili tuweze kumpata Mungu ni lazima tumtafute kwa bidii.Na pia Mungu ametuahidi kuwa tukimtafuta kwa bidii tutampata.Watu wa Mungu tukumbuke kwamba yote tunayoyatafuta hapa duniani,Mungu anaweza kutupatia kwani fedha na dahhabu ni mali zake.Tunaona hapo mstari wa 18,anasema,utajiri na heshima ziko kwake,tena vyote,utajiri na kila kitu ni vya kudumu.
Wakristo tujiulize kwanini wengi wetu ni masikini?.Kama neno la Mungu hapo juu linamajibu yote,inatupasa tumrudie Mungu,tumtafute kwa bidii kisha tutapata vyote.

SALA

Mungu asante kwa ujumbe wa Neno lako lenye kutubariki.Tunakuomba utushushie neema yako ya kulijua na kulitafakari neno lako ili tubarikiwe kwa kupitia ufahamu wa neno hili.Hakika hatutaweza kufanikiwa kama hatutakaa ndani yako nawe ukatupa sehemu ya unavyo vimiliki,kwani neno litnatutaka tukutafute kwa bidii.Ni kaitika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo tumeomba.Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | (AMEFUFUKA KWELI!!) | MATHAYO 25:40.Na mfalme atajibu,akiwaambia,Amin nawaambia,kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu,walio wadogo mlinitendea mimi…

MATHAYO 25:40

Na mfalme atajibu,akiwaambia,Amin nawaambia,kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu,walio wadogo mlinitendea mimi.

TAFAKARI

Watu wa Mungu tunaona jinsi ambavyo matendo yetu kwa watu wengine yalivyo na maana mbele za Mungu.Tunaweza kufanya jambo kwa mtu/watu,nakudhani litaishia nafsini mwetu lakini kumbe linamwendea Mungu kama lilivyo.Hivyo basi watu wa Mungu tujitahidi kuwatendea wengine mema ili tumbariki Mungu.Tukumbuke kuwa kila mema tunayotenda yanakwenda kuwa hazina yetu Mbinguni.Tumrudieni Mungu na kutenda yanayo mpendeza.

SALA

Bwana wetu Yesu Kristo,tunakushukuru kwa kufa na kufufuka ili tukombolewe na kuwa na uzima.Hatuna chakukulipa ila tunaupokea wema wako.Wewe ni mwema sana,wala hauna wakulinganishwa naye.Tumelisikia neno la leo zuri lenye kutubariki.Tunakuomba utupe hekima ya kuliweka mioyoni mwetu na kulitenda ili sifa na utukufu vikurudie wewe.Ni katika Jina la Yesu Kristo tumeomba.Amen.
©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | IJUMAA KUU | Luka 23: 13-14 Na Pilato akawakutanisha wakuu wa makuhani, na wakubwa, na watu akawaambia, Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu…

IJUMAA KUU

Luka 23: 13-14
Na Pilato akawakutanisha wakuu wa makuhani, na wakubwa, na watu, akawaambia, Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua mambo yake mbele yenu, ila sikuona kwake kosa lo lote katika mambo hayo mliyomshitaki

TAFAKARI

Leo ni Ijumaa kuu. Tunajiunga na wakristo wote Duniani kukumbuka siku Bwana wetu Yesu Kristo alivyoteswa na kufa msalabani kwa sababu ya kutuokoa katika dhambi. Neno la leo linasisitiza kuwa Bwana Yesu hakusulubishwa msalabani kwa sababu ya makosa aliyotenda. Pilato alikuwa yuko tayari kumuachia huru lakini ili maandiko yatimie ilibidi asulubishwe msalabani ili mimi na wewe tupate nafasi katika uzima wa milele. Bwana Yesu alishafanya kazi yake, kazi iliyobakia sasa ni kwa wewe na mimi kumpokea Yeye(bwana Yesu) katika maisha yetu ili atuongoze katika safari hii ndefu ya kwenda mbinguni.

SALA

Mwenyezi Mungu baba wa rehema,tunakushukuru kuwa umetuweka salama mpaka leo hii tumeweza kuiona Ijumaa kuu hii . Tunakuomba uzidi kutulinda na kutuongoza katika ile njia ya haki ili tuweze kuuona uufalme wako. Tunaomba haya katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Ameen

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org