NENO LA LEO | MATHAYO MTAKATIFU 11:4-6 Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayosikia na kuyaona; vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa,viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na masikini wanahubiriwa habari njema…

MATHAYO MTAKATIFU 11:4-6

Yesu akajibu akawaambia,Nendeni mkamweleze Yohana mnayosikia na kuyaona;vipofu wanapata kuona,viwete wanakwenda,wenye ukoma wanatakaswa,viziwi wanasikia,wafu wanafufuliwa,na masikini wanahubiriwa habari njema.

TAFAKARI

Jiulize,pamoja na Bwana wetu Yesu Kristo kufanya miujiza MINGI,ya kuokoa,viziwi kuona,wafu kufufuliwa na mengine yote MAKUU;Lakini bado alidhihakiwa,akateswa,akasulubiwa msalabani,na kisha akafa.Yote hayo haikuwa kwasababu alitenda dhambi ila tuu ni kwasababu ya upendo wake USIO ELEZEKA kwa ufahamu wetu binadamu.Watu wa Mungu tuchukueni hatua ya kutafakari kwa kina MATENDO Makuu ya Bwana wetu Yesu Kristo aliyo tufanyia,kisha TUCHUKUE hatua za kubadilika na kutubu ili SIKU ya mwisho wa maisha yetu tukakae na Bwana Yesu katika kiti cha Enzi tukiwa na furaha isiyo na kifani.

SALA

Mungu wetu,asante kwa siku nyingine tena hii katika maisha uliyotupa.Tunarudisha sifa na shukrani zetu kwako kwa kila ulilotujalia.Tuna kuomba utujalie ufahamu wa upendo wapekee ambao Bwana wetu Yesu Kristo alitufanyia pale msalabani.Hatuna chakumlipa zaidi ya kusema asante na pia kutenda mema siku zote za maisha yetu.Ni katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo,tumeomba.Amen

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | MATHAYO MTAKATIFU 26:1-2 Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake, Mnajua yakuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, na Mwana wa Adam atasalitiwa asulubiwe…

MATHAYO MTAKATIFU 26:1-2

Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo yote,aliwaambia wanafunzi wake,Mnajua yakuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka,na Mwana wa Adam atasalitiwa asulubiwe.

TAFAKARI

Tuanaona Bwana wetu Yesu Kristo anawaambia wanafunzi wake jinsi atakavyo sulubiwa ili PASAKA iweze kudhihirika.Ila anawaambia ili Pasaka idhihirike ni lazima akamatwe na kusulubiwa.Na ili asulubiwe ni lazima ASALITIWE.Tunaona kwamba Dhambi ilikuja kabla ya Ushindi wa Bwana wetu Yesu Kristo,na walioileta hiyo dhambi ni sisi wanadamu.Hivyo Watu wa MUNGU tujue kuwa tunapotenda dhambi ni kosa kubwa sana kwa Mungu.Kama siyo dhambi Bwana yesu asingekufa msalabani.Hivyo tuache dhambi ili tuuchuchumilie UZIMA wa Milele.

SALA

Baba uketiye katika kiti cha enzi.Asante kwa jinsi ulivyo mkuu.Asante kwa uhai ulotupa hata kufikia siku ya leo.Asante kwa vyakula,vinywaji na kila kitu.Asante kwa neno lako takatifu.Tunakuomba ufumbue uelewa wetu ili tukae ndani yako siku zote za maisha yetu na mwisho wa yote tukaurithi uzima wa Milele.Ni katika Jina la Yesu Kristo tumeomba. Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO | LUKA MTAKATIFU 6:20-21. Akayainua macho yake akawatazama wanafunzi wake, akasema, Heri ninyi mlio masikini, kwasababu ufalme wa Mungu ni wenu…

LUKA MTAKATIFU 6:20-21

Akayainua macho yake akawatazama wanafunzi wake,akasema,Heri ninyi mlio masikini,kwasababu ufalme wa Mungu ni wenu.Heri ninyi mlio na njaa sasa,kwasababu mtashiba,Heri ninyi mliao sasa,kwasababu mtacheka.

TAFAKARI

Tunaona jinsi Neno linavyozungumzia jinsi watu wanaopitia kwenye mambo magumu lakini wanaendelea kumtumaini Mungu na kuzidi kukaa ndani yake.Tunaona kwamba ili kuweza kupata mema ambayo Mungu ametuandalia ,wakati mwingine tunapitia kwenye mambo magumu kiasi cha kufikia hata kulia,au kwenye umasikini,au wanaopitia kwenye njaa Kwa ajili ya UFALME wa Mbinguni.Wakristo tusiogope majaribu yanapokuja,tumtumainie Mungu na kukaa ndani yake kwani mwisho wake ni mwema kulingana na MAANDIKO matakatifu ya Mungu.

SALA

Asante Mungu mwema kwa neno lako takatifu linalotubariki.Tunakuomba utupe neema na karama ya kulijua na kuliheshimu neno lako.Na pia hata tukikutana na majaribu kiasi gani tusikuache ila tuzidi kudumu ndani yako hata ukamilifu wa dahari.Ni katika jina la bwana wetu Yesu Kristo tumeomba.Amen.

©IYK-NENO
www.iykcolumbus.org