NENO LA LEO | Yoshua 1:3 Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.

Yoshua 1:3 Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.

TAFAKARI: Maandiko yanatufundisha kuwa Mbingu ni Nchi ni mali ya Bwana. Tena yanasema mbinguni ni kwake Mungu lakini nchi amewapa wanadamu waishi; kisha Fedha na dhahabu yote pia ni mali yake.
(Zaburi 24:1,115:16, Hagai 2:8)
Kwa kuwa vyote ni vya kwake, alimpa Abraham urithi wa nchi ili iwe yake yeye na vizazi vyake hata milele. Leo hii Mungu amekuweka wewe kwenye hii nchi kwa kusudi. Leo hii ungeweza kuwa pahala popote duniani lakini upo hapa maana Mungu ameamuru uwepo. Nataka nikutie moyo kuwa usiogope ndugu yangu. Mwamini Mungu katika yote ufanyayo. Naamini kwa moyo wangu wote Mungu anataka ufanikiwe, Mungu anataka uwe na afya njema na maisha mazuri. Kama unapambana bado na shida, siku ya leo liite Jina la Bwana Mungu wako. Mkumbushe akupe ile baraka aliyokuandalia katika nchi hii. Hata kama unaona umebarikiwa katika maeneo mengi basi usiache kumwita akutembelee katika maeneo yale yote uliyopungukiwa.

SALA: Mungu wangu, kutana na mahitaji yangu siku ya leo. Naomba uje upate kufuta yale machozi yangu ya sirini. Kutana na ile haja ya moyo wangu ili nipate kukutukuza wewe daima. kwa Jina la Yesu nimeomba,  Amina.
(c)IYK_Neno
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO: Zaburi 109: 1-5 Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze,. . .

NENO LA LEO: Zaburi 109: 1-5 Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze, Kwa maana wamenifumbulia kinywa; Kinywa cha mtu asiye haki, cha hila, Wamesema nami kwa ulimi wa uongo. 
Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka, Wamepigana nami bure.Badala ya upendo wangu wao hunishitaki, Ijapokuwa naliwaombea. Wamenichukuza mabaya badala ya mema, Na chuki badala ya upendo wangu. 
TAFAKARI:Wakati mwingine binadamu watakulipa mabaya japokuwa wewe unawatendea mema. Watakusengenya na kutaka kukuharibia maisha yako kabisa pamoja na kwamba uliwasaidia. Wakati mwingine inakuwa ni wivu tu na wakati mwingine inakuwa ni chuki tu zisizo na msingi wowote. Mwimba zaburi anatufundisha kuwa kwa Mungu hakuna linaloshindikana. Hivyo kila mara tunapokuwa katika matatizo tumlilie Mungu. Tumuite Mungu naye atatuitika (yeremiah 33:3)
SALA: Baba Mungu tunakuita utusimamie katika safari yetu hapa duniani kwa sababu shetani haishi kutuingilia watumishi wako na kutaka kututenganisha sisi na wewe. Utulinde ili maadui zetu wajue kuwa sisi tunamtumaini Mungu aliye hai ambaye kwake hakuna linaloshindikana. AMEN!
(c)IYK_Neno

NENO LA LEO: Zaburi 37:39, Na wokovu wa wenye haki una Bwana…

NENO LA LEO: Zaburi 37:39, Na wokovu wa wenye haki una Bwana; Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.
TAFAKARI: Inawezekana unapitia kwenye shida muda huu, mambo yako hayaeleweki na una hofu ya mambo mengi. Labda una mtu wako wa karibu ambaye anasumbuliwa na ugonjwa ambao kwa namna moja au nyingine unatishia maisha yake. Nataka nikutie moyo kuwa wakovu wa wenye haki una Bwana; Yeye ni ngome yao wakati wa taabu. Nataka nikutie moyo kuwa mwendee Mungu, mkimbilie yeye siku ya leo. Mwambie unachopitia, mwombe akusadie, yeye atakutia nguvu katika kipindi chote kigumu unachopitia na atakusadia kushinda yote yanayokusumbua.
SALA: Mungu wangu, naomba unisadie niweze kushinda majaribu ninayo pitia . Kutana na shida na matatizo yangu, nipiganie ili niweze kushinda vyote sawa sawa na Neno lako linavyosema. Kwa Jina la Yesu, Amina.
(c)IYK_Neno
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO: 1 SAMWELI 18 :8 – 9 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema,…

NENO LA LEO: 1 SAMWELI 18 :8 – 9  Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa DAUD makumi elfu, na MIMI wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni UFALME? Sauli akamwonea Daudi WIVU tangu siku ile.

TAFAKARI: WIVU ni dhambi, na wala siyo TABIA ya Kikristo.Yawezekana dhambi hii ya wivu ikaonekana kuwa SIYO dhambi kubwa mbele ya macho ya MWANADAMU. Katika hali halisi, dhambi ya WIVU ina MADHARA makubwa maishani mwetu. “SAULI akaghadhibika sana …akamwonea DAUD wivu tangu siku ile” Wivu una UWEZO wa kuvunja mahusiano ya marafiki, ndugu, wanandoa, hata wanajamii. Je! MKRISTO awezaje kuishinda dhambi hii ya WIVU? Katika injili ya Mathayo 5:43 – 44, Bwana Yesu anatufundisha kuwa UPENDO na MAOMBI ndiyo njia BORA za kuishinda dhambi ya WIVU. Yesu asema, “ wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.”
Mungu peke yake ndiye mwenye HAKI ya kuwa na wivu. (Nahumu 1:2 ) “Bwana ni Mungu mwenye wivu,
naye hujilipiza kisasi….juu ya adui zake.” WIVU wa Mungu una NIA njema. Wivu wa Mungu una DHUMUNI la kuiondoa DHAMBI na kuleta UPATANISHO, (Kumbukumbu 5:9)
Mungu na atusaidie ili tuweze kujihadhari kwa kutoiruhusu dhambi ya wivu maishani mwetu.

SALA: Mungu wa Mbinguni, tunakuomba utujaze na pendo lako la AGAPE ili tuweze kuishinda dhambi ya wivu maishani mwetu, ni katika Jina la Yesu Kristo,
tunaomba, utusikie, amina.
(c)IYK_Neno