NENO LA LEO: Zaburi 35:1-3, Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami. . .

NENO LA LEO: Zaburi 35:1-3, Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami. Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie. Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia, Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako. 
TAFAKARI: Mara nyingi tunapenda kuchukua mambo mikononi na kupigana vita zetu sisi wenyewe. Tunasema tumempokea Yesu na tunaishi maisha matakatifu. Lakini pindi watu wanapoanza kutusema au kutupinga katika mambo fulani. Huwa tunainuka na kuanza kurudisha mashambulizi huku tukiwalipa kama vile walivyotutendea. Haipaswi kuwa hivyo, Mzaburi alimgeukia Bwana pindi pale watu walipomsema na akaomba kuwa Bwana atete nao. Pindi watu walipoinuka kupigana nae, aliomba Bwana ndio apigane nao na amsadie kumshindia. Alijua kuwa wokovu wake watoka kwa Bwana, na alimkabidhi yote yeye na sisi imetupasa tumkabidhi yote Yesu na yeye ndo atashughulika na watesi wetu.
SALA: Mungu wangu naomba utete nao wanaoteta nami, upigane nao wanaopigana nami. Uishike ngao na kigao, Usimame unisadie katika vita zangu zote ee Bwana. Kwa Jina la Yesu, Amina.
(c)IYK_Neno

NENO LA LEO: Wafilipi 4:19, Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake. . .

NENO LA LEO: Wafilipi 4:19, Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. 
TAFAKARI: Moja wapo ya kitu nilicho jifunza katika maisha yangu wokovu ni kwamba Mungu anajua tuna mahitaji na yupo kwa ajili ya kutimiza maihitaji yetu. Nimejifunza kuwa Mungu anataka tuishi kwa imani na kufuata kanununi zote ambazo maandiko yanatufundisha. Mfano kutoa zaka na sadaka kwenye nyumba yake. Pindi tunapotembea katika hizi kanuni na kuishi kwa imani ndani ya Yesu. Mungu hufungua milango ya baraka kwetu na kutuza kwa kila tunachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. Hutupa kibali kuliko wengine, na kuhakikisha kuwa anabariki kazi za mikono yetu na kufungua madirisha ya mbinguni ili tupate kupokea baraka toka kwake.
SALA: Mungu wangu, naleta mahitaji yangu mbele zako. Naomba ukutane na kila hitaji langu kwa kadiri ya utajiri wako, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. Kwa Jina la Yesu, Amina.
(c)IYK_Neno

NENO LA LEO: Mwanzo 3:12 – 13 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo…

NENO LA LEO: Mwanzo 3:12 – 13 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.

TAFAKARI: Mungu wetu SIYO Mungu wa LAWAMA.  Tangu mwanzoni, MWANADAMU alipoamua kuisikiliza SAUTI ya shetani, dhambi ya
LAWAMA iliyatawala maisha yake.  Somo la leo, linamshuhudia baba yetu Adamu, anavyomlaumu MUNGU. “…huyu MWANAMKE uliyenipa …ndiye aliyenipa MATUNDA ya mti huo, NIKALA.  Mama yetu Eva, kama vile Adamu, naye AKAMLAUMU, nyoka “ …nyoka alinidanganya, NIKALA.”
Matokeo ya dhambi ya LAWAMA ni ADHABU ya MAUTI.  Dhambi hii imeendelea kukisumbua hata kizazi cha leo.  Mungu wetu hafurahishwi na LAWAMA zetu. Kwa MOYO wa UPOLE na kwa MACHOZI yenye HURUMA, Mungu aliamua kutufia juu ya MSALABA. Msalaba unaoturudisha ndani
ya EDENI mpya; yaani, maisha ya WOKOVU! Msalaba huu, unatuokoa dhidi ya nguvu ya DHAMBI, KIFO, na SHETANI, amina.

SALA: Ee Mungu wetu, tunakuomba utupe nguvu ya kumshinda shetani na kazi zake zote.  Utusaidie ili tuyatende mapenzi yako
maishani mwetu, ni katika Jina la Yesu Kristo, Amina .
(c)IYK_Neno
www.iykcolumbus.org

NENO LA LEO: Zaburi 99:6-8, Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake,

NENO LA LEO:  Zaburi 99:6-8, Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake, Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake, Walipomwita Bwana aliwaitikia; Katika nguzo ya wingu alikuwa akisema nao. Walishika shuhuda zake na amri aliyowapa. Ee Bwana, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu; Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe Ingawa uliwapatiliza matendo yao.
TAFAKARI: Mungu wetu ni Mungu mwenye kusamehe. Kila itwapo leo hutuma watumishi wake katika kila kona ya ulimwengu kwa namna tofauti tofauti wapate kufikisha huu ujumbe wa msahama kwa wanadamu. Huyu Mungu hajaanza leo kusamehe, alifanya hivyo hata kipindi cha Agano la kale na aliwasamehe watumishi wake na watu wote walimwendea kwake wakiwa na moyo wa toba. Kuna wengi wanadhani kuwa dhambi na maovu yao ni mengi kiasi ambacho Mungu hawezi kuwasamehe. Wanafikiri kuwa Mungu anawachukia na hawezi tena kuwarehemu. Maandiko yapo wazi kuwa dhambi zetu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama bendera, zitapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu kama tutazitubu, Isaya 1:18. Nakusihi uende mbele za Mungu na ukatubu kwa pale ambapo una shuhudiwa ndani ya moyo wako kufanya hivyo. Mungu ni mwenye huruma na atakusamehe kabisa.
SALA: Mungu wangu, naomba nisamehe kwa dhambi na maovu yangu yote. Futa jina langu katika kitabu cha hukumu na liandike kwa upya kwenye kitabu cha hukumu. Kwa Jina la Yesu, Amina.
(c)IYK_Neno
www.iykcolumbus.org